Sunday, November 16, 2014

Haya ndio maua ya ndani mazuri kwa afya yako




nephytis


spider plant


dwarf date palm



sword fern

Lady palm

Maua nyumbani au ofisini sio mapambo tu bali ni mazuri kwa afya yako kwani husafisha hewa na kufanya mazingira yako ya nyumbani au ofisini kupendeza kufanyia kazi au kuishi.Kwa hiyo wewe kama sio mpenzi sana wa kupamba basi pata ua (au yote) kati ya hayo juu japo kwa nia ya kuboresha hewa ya nyumbani kwako au ofisini. Kama una watoto wadogo au wanyama kama paka au mbwa ni muhimu kuhakikisha hawachezei maana maua mengine yanaweza yakawadhuru wakiyala. Pia kuna maua zaidi yafanyayo kazi hii majina yake hapa na hapa ila haya nimeona ni post haya maana yanapatika kirahisi kwetu na utunzaji wake sio mgumu. Tuzipende afya zetu na sehemu tunazoishi,Enjoy!

Saturday, November 15, 2014

Watoto wazungumza lugha isiofahamika



Watoto wamekaa na mamayao wakila chakula.nchini Uganda watoto watatu waliofungiwa na baba yao kwa miaka saba wameanza kuzungumza lugha isiofahamika.
Watoto watatu kutoka kijiji cha Barca katika kaunti ndogo ya Aber Wilayani Oyam nchini Uganda wameanza kuzungumza lugha tofauti isiojulikana baada ya kufungiwa katika nyumba kwa miaka saba.
Lugha hiyo mpya imetajwa kuwa Leb -adam ikimaanisha lugha ya ubongo na jamii ya eneo hilo.
Inadaiwa kuwa baba ya watoto hao aliwafungia ili kuwalinda kutokana na hatari yoyote.
Kulingana ma gazeti la the monitor nchini Uganda,watoto hao hawajaathirika kiakili lakini hawawezi kuzungumza na watu wengine.Wanaamini tu kile baba yao anachowaambia.
Kulingana na mama yao watoto hao waliweza kuishi kwa kula mayai ya chura yaliochemshwa na majani,ambayo hula kila asubuhi na jioni na hutumia maji kutoka shimo lililochimbwa na baba yao.
Mama yao anasema kuwa baba ya watoto hao alimzuia kutozungumza nao hatua iliowafanya kutojifunza lugha ya kiluo wakati walipokuwa wadogo.
Mwanamke huyo amesema kuwa alionywa na baba huyo kutosema chochote kuhusu watoto hao.

Umesikia kuhusu mwanamke aliyekaa Mochwari kwa saa 11?



jokofuuuuuuuuuu
Story za maajabu ya ulimwengu zinaendelea kukaa kwenye headlines kila siku, na inaponifikia cha kwanza ninachokifanya ni kukufikishia mapema iwezekanavyo ili na wewe usipitwe.
Ya leo inaweza kuwa moja kati ya zilizowahi kukushangaza zaidi, inahusu mwanamke Janina Kolkiewicz raia wa Poland, mwenye umri wa miaka 91 ambaye amekaa kwa muda saa 11 katika chumba cha kuhifadhia maiti huku mwili wake ukiwa ndani ya jokofu baada ya kuthibitishwa na daktari wa familia yake kwamba amefariki, muda mfupi baadaye wahudumu wa mochwari waligundua kwamba ni mzima baada ya kuhisi anatikisika ndani ya mfuko alimowekwa.
Baada ya kurudi nyumbani kwake akitokea mochwari, alilalamika kuhisi baridi kali na kupatiwa bakuli la supu ya moto na mkate.
Daktari aliyethibitisha mauti ya mtu huyo anasema hata yeye anashangazwa na tukio hilo kwani vipimo vyote vilionyesha kuwa mapigo ya moyo yalisimama na hakuwa hai.
Taarifa za kuwa hai mwanamke huyo zilimshtua kila mtu kwenye familia yake na kujikuta ikibatilisha hati ya kifo iliyotolewa kwa ajili ya mazishi yake ambayo yalipangwa kufanyika siku mbili baadaye..

Tazama picha za mtu mrefu zaidi na mtu mfupi zaidi Duniani walipokutana kwa mara ya Kwanza.


Tall III
Tumekuwa tukisikia rekodi mbalimbali zikivunjwa na watu duniani na rekodi hizo maalumu huwa zinatunzwa katika kitabu cha kumbukumbu cha Guiness World Records.
Kwa mara ya kwanza, watu ambao wako katika kitabu hicho kutokana na kuvunja rekodi hizo za kipekee wamekutana London Uingereza siku ya Novemba 13.
Chandra Bahadur Dangi mtu aliyevunja rekodi ya kuwa mtu mfupi kuliko wote Duniani amekutana kwa mara ya kwanza na Sultan Kosen, jamaa ambaye amevunja rekodi ya kuwa mtu mrefu zaidi duniani.
Chandra anatokea Nepal ana urefu cha Sm. 54.6, Sultan anatokea Uturuki ana urefu wa Sm. 251 ambayo ni sawa na futi 8.3.
Hizi ni picha zinazowaonyesha wakali hao wakiwa pamoja.
Tall II
Tall & Short
Tall IV
Tall III
Tall V
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Huyu Jamaa hataki chakula lakini anakula vipande vya matofali kila siku


3Mama yake  huwa anamuandalia wali kama chakula cha siku lakini anakataa na kutaka apewe vipande vya matofali.
Kwa siku moja anakula vipande kadhaa vya matofali ambapo kwa makadirio huwa anakula kilo 3 kila siku.
Fundi huyo wa kujenga nyumba Pakkirappa Hunagundi anasema kwamba ameanza kula vitu kama hivyo tangu akiwa na miaka 10 na anaweza kukosa chakula lakini hawezi kukosa kula vipande vya matofali.
Akiwa anapata chakula chake hicho akipendacho(matofali) huwa anahitaji kikombe cha maji tu ili kushushia na mwenyewe anasisitiza kwamba hajisikii tofauti kabisa.
Mkazi huyo wa kijiji cha Karnataka nchini India anasema anataka kuzunguka India nzima akionyesha watu uwezo wake huo na kujipatia pesa kwa kuonyesha maajabu hayo.

2
a
1
b